Thursday, May 08, 2025

SERIKALI KUENDELEA NA URASIMISHAJI MAKAZI KINONDONI





Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ardhi inaendelea kutekeleza mpango wa urasimishaji wa makazi katika halmashauri ya manispaa ya Kinondoni ambapo hadi sasa mitaa 33 kati ya 53 imekwisha fikiwa.

Pinda amesema hayo leo Mei 8, 2025 bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Abbas G. Tarimba Mbunge wa Jimbo la Kinondoni aliyeuliza Je! Lini Serikali itakamilisha zoezi la urasimishaji makazi katika Jimbo la Kinondoni?.

Aidha Mhe. Pinda amesema kuwa makazi 60,436 yametambuliwa na kurasimishwa na Jumla ya hatimiliki za ardhi 11,026 zimetolewa kwa wananchi hadi sasa.

Vilevile, Pinda amesema kuwa Halmashauri ya Kinondoni ni miongoni mwa manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam ambazo hadi sasa mitaa 270 za mkoa huo zinahitaji kiasi cha Bilioni 3.3 ili kukamilisha zoezi la Urasimishaji.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatarajia kukamilisha zoezi hili la urasimishaji kadri fedha zitakavyokuwa zikitengwa katika bajeti za Wizara.

No comments:

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA VIFAA TIBA NCHINI ITALIA

ROMA, ITALIA – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, ametembelea kampuni ya kimataifa ya uzalis...