Monday, October 14, 2024

TARI KUENDELEZA KILIMO CHA KULINDA MAZINGIRA NA KUCHANGIA USALAMA WA UCHUMI WA BLUU

 

Meja Generali Steven Mkande akimkabidhi zawadi ya Ngao kwa kituo Cha Utafiti Mlingano pamoja na Ngao kwa Taasisi ya Tafiti Tanzania  (TARI) wa  Mkurugenzi wa Uhulishaji wa teknolojia na mahusiano wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Sophia Kashenge.

Na Lucas Raphael,Tanga

Mkurugenzi wa Uhulishaji wa teknolojia na mahusiano wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Sophia Kashenge amesema TARI inaendeleza tafiti za kilimo cha kulinda mazingira na ikolojia ya bahari hivyo kuchangia uchumi wa bluu.

Alitoa kauli hiyo wakati akitoa mada maalumu kwa maafisa wanafunzi na viongozi wa juu wa jeshi wa chuo cha kijeshi Duruti Arusha kwa  mwaka 2024/25 wanaotoka katika nchi 23 za Afrika.

Dkt. Sophia kashenge alitoa  mada  maalum  kwa maafisa hao  kwa niaba ya  Mkurugenzi Mkuu wa  TARI Dkt. Thomas Bwana  alisema Jeshi ili liweze kulinda amani ya Nchi vizuri lazima kuwepo na usalama wa chakula kwa wananchi na hakuna usalama wa chakula bila usalama wa teknolojia mbalimbali zinazoweza kuongeza uzalishaji wa chakula ikiwemo usalama wa mbegu.

Alisema TARI ina mchango mkubwa katika kufanya tafiti zinazolenga kuwa na usalama wa chakula na hivyo kulisaidia Jeshi ulinzi wa nchi kwa kuwa na chakula cha kutosha na kusisitiza kwamba ni vigumu kutawala wananchi wenye njaa.

Alisema utafiti unaofanywa na TARI unamuunganiko wa moja kwa moja katika kusaidia kulinda ikolojia ya bahari na kuchangia katika uchumi wa bluu.

“Akitoa  Mfano wa matumizi sahihi ya mbolea na viwatilifi, unapozidisha mbolea na viwatilifu athari zake hupelekwa baharini kupitia mito na mafuriko hivyo Tafiti za kulinda mazingira hupunguza  hewa ya ukaa ambayo inapozidi huingia baharini na kuchangia mabadiliko ya sifa ya maji ya bahari na kuathiri sana mimea na viumbe bahari” alisema Dkt. Sophia.

Alisema utafiti wa TARI unalenga zaidi kuboresha mazingira ya bara hali ambayo inapunguza sumu na udongo kumomonyoka kuelekea baharini.

Dkt. Sophia alisema Msingi mkuu wa utafiti wa TARI ni kuendeleza kilimo cha kulinda mazingira ili kuepukana na mabadiliko ya tabia Nchi yanayoleta changamoto mbalimbali za kimazingira, kiafya pamoja na changamoto za kiusalama.

Alisema Taasisi hiyo itaendelea kufanya tafiti na kuzipeleka kwa wananchi ili kulinda mazingira yote ya Nchi kavu na mazingira ya Baharini hasa Uchumi wa bluu ambao ni muhimu kwa mahitaji ya binadamu.

Aidha mkuu wa chuo cha kijeshi Arusha  Meja Generali Steven Mkande aliipongeza Taasisi ya TARI Chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt Thomas Bwana , pamoja na Kituo cha mlingano kwa kutuonesha jinsi gani wagani wanavyofanya utafiti kwa ajili ya kuchochea na kusukuma maendelea ya nchi .

Aidha alisema kwamba wanashukuru kupata elimu iliyotewa na Dkt Sophia kwa wasilisho mazur ambayo yametoa funzo kubwa kwa wajeshi juu ya  Tafiti za kilimo zinavyosaidia usalama wa ikolojia ya bahari na kuchangia uchumi wa bluu jambo ambalo linamuunganiko katika kuongeza usalama wa chakula na kuchangia usalama wa nchi kwa ujumla 

Alisema Mafunzo hayo yatawasaidia wanajeshi ili  waweze kuzilinda vyema Nchi sambamba na kulinda Mazingira lengo likiwa na kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi na ukosefu wa usalama na Amani katika baadhi ya nchi.

Katika Mafunzo hayo Meja Jenerali  Mkande alikabidhi zawadi ya Ngao kwa kituo Cha Utafiti Mlingano pamoja na Ngao kwa Taasisi ya Tafiti Tanzania  (TARI).

Chuo hicho kilichopo eneo la Duluti mjini Arusha kinatoa mafunzo ya kila mwaka kwa wanajeshi  wa ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. 

Wanajeshi hao walipata fursa ya kutembelea kituo cha TARI Mlingano mkoani Tanga na shughuli mbalimbal zinazofanywa na taasisi hiyo ya kilimo nchini

Aidha katika mafunzo hayo wanajeshi hao walipara  fursa ya kutembelea taasisi mbalimbali na kujifunza jinsi taasisi hizo na kazi zake zinavyochangia amani na  usalama wa nchi na bara zima la Afrika.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...