Na Mwandishi Wetu
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata faida kabla ya kodi na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 199.3 ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Hayo yamesemwa leo (Oktoba 13, 2024 )na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah alipokuwa akizungumza na Viongozi mbalimbali wapatao 1,000 wa Wilaya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lengo na Mkutano likiwa ni kuelezea mafanikio na mizania ya Shirika kwa mwaka 2023/2024 na kuelezea mwelekeo wa Shirika kwa Mwaka 2025 katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-25
"Shirika limeendelea kuongeza faida kabla ya kodi na kufikia kiasi cha shilingi bilioni 42.25 sawa na asilimia 147 ya lengo.Miradi ya Kihistoria Kuinua Taswira ya Ilala
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu alisisitiza kuwa Ilala ni miongoni mwa maeneo muhimu ambapo NHC inatekeleza miradi mingi ya kihistoria kupitia Sera ya Ubia. Alieleza kuwa juhudi hizo tayari zimeanza kuzaa matunda na kubadilisha muonekano wa eneo hilo.
"Ilala inakwenda kuwa kama Dubai. Tunajenga miradi inayozingatia kasi na viwango vya kimataifa. Tukijipa miaka 10 ijayo, Ilala itakuwa imejipa historia ya kutoonekana majengo mabovu," alisema kwa matumaini makubwa Mkurugenzi Mkuu.
Uongozi Bora na Thamani ya Mali za NHC
Aliongeza kuwa thamani ya mali za NHC imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, kutokana na usimamizi madhubuti na maelekezo bora kutoka serikalini na chama tawala. Uimarishaji wa usimamizi umechangia kuongeza thamani ya mali na kuimarisha nafasi ya NHC kama mchezaji mkubwa katika sekta ya nyumba na uwekezaji nchini.
Katika hatua nyingine amesema kuwa, ndani ya miaka mitano kuanzia 2018/19-2023/24 mapato ya shirika yamekuwa kutoka shilingi bilioni 125 kwa mwaka hadi shilingi bilioni 184 kwa mwaka sawa na ongezeko la asilimia 47 kwa mwaka.
"Mapato ya mwaka 2023/24 ambayo yanaendelea kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali yamefikia shilingi bilioni 184."
Aidha, amewaeleza viongozi hao kuwa, majukumu ya shirika hilo yanatekelezwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa NHC ambao ulianza 2015/16 -2024/2025.
Pia amesema, thamani na mali za shirika zinaendelea kukuwa mwaka hadi mwaka kutokana na usimamizi na maelekezo mazuri wanayopata kutoka serikalini na chama tawala.
Mkurugenzi Mkuu huyo ameyasema hayo leo Oktoba 13,2024 katika wasilisho lake kuhusu majukumu na mafanikio ya shirika hilo katika mkutano wa viongozi wa Jimbo la Ilala mkoani Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment