NA MWANDISHI WETU
KATIKA
kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Benki ya NMB imeitambulisha
kampeni kubwa ya mapinduzi huduma kiteknolojia iitwayo Sisi ni Huduma
‘Tumekupata,’ utambulisho uliofanyika sambamba na uzinduzi wa Mtoa
Huduma wa Kidigitali ‘Chatbot’ aliyepewa jina la NMB JIRANI.
Utambulisho
na uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Oktoba 7,
ambako Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema Huduma kwa
Wateja ni Ajenda ya Kimkakati, inayohitaji uwekezaji wa hali ya juu kwa
wafanyakazi na teknolojia ili kuendana na kasi ya kukua kwa taasisi yake
hiyo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Bi. Zaipuna
alisema katika kukidhi mahitaji ya wateja zaidi ya milioni 8 wa benki
hiyo Sisi ni Huduma na NMB JIRANI inaenda kuleta masuluhisho mbalimbali
kwa wateja na wasio wateja wao.
“NMB
ni benki inayokua kwa kasi sana na hili limetusukuma kuifanya Huduma
kwa Wateja kuwa ni Ajenda ya Kimkakati, mafanikio tuliyoyapata katika
miaka mitano ya karibuni, yametusukuma kuyaangalia mafanikio hayo kwa
namna ambavyo benki imegusa maisha ya watu kijamii na kiuchumi.
“Takwimu
zinaonesha kuwa mikopo kwa wateja wa NMB imeongezeka sana tangu mwaka
2019 ilipokuwa Sh. Trilioni 3.6 hadi Sh. Trilioni 8 mwaka huu wa 2024
iliyoenda katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, uvuvi, ufugaji,
viwanda, biashara, mashirika na watu binafsi, kwahiyo tukahitaji kutanua
wigo wa kuwahudumia.
“Benki
imekuwa kwa kasi kimtandao, unaojumuisha matawi 231, mawakala
wanaongezeka kutoka 6,000 mwaka 2019 hadi 44,000 hivi sasa, pia tulikuwa
na akaunti za wateja milioni 3 mwaka 2019 na sasa zimefikia milioni 8.
Menejimenti tukatafakari namna gani ya kuiendesha benki inayokuwa kwa
kasi kama hii.
“Tukaona
tufanye mapinduzi makubwa katika huduma kwa wateja na kuifanya hii kuwa
ni Ajenda ya Kimkakati na unapoweka ajenda ya kimkakati, unahitiaji
uwekezaji wa hali ya juu kwa wafanyakazi na teknolojia, hivyo mafunzo ya
ndani miezi mitatu iliyopita na leo tunazindua kampeni hii pamoja na
NMB JIRANI.
Bi
Zaipuna akaongeza ya kuwa, hakutakuwa na gharama yoyote kuhudumiwa na
NMB JIRANI, bidhaa iliyotokana na ukweli kuwa changamoto kubwa
wanayopitia watoa huduma ikiwemo NMB ni maswali kutoka kwa wateja,
ambapo Vituo vya Huduma kwa Wateja vimeshindwa kumaliza hilo kutokana na
kuelemewa.
“Njia
pekee ya kumaliza maswali ya wateja ilikuwa ni Vituo vya Huduma kwa
Wateja, ambavyo mara kadhaa vimezidiwa, tukaona tuje na NMB JIRANI,
ambaye ni muhudumu kwa njia ya kidijitali, atakayejibu maswali ya wateja
na hata wasio wateja wetu.
“Iwe
maswali kuhusu huduma zetu na masuluhisho yetu, ambako mteja ataingia
kwenye tovuti yetu ya www.nmbbank.co.tz eneo la TUTAFUTE au kupitia
mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp (0747 333 444), kisha JIRANI
atajibu maswali kuhusu thamani ya pesa za kigeni, bima, mikopo na
mengineyo.
Aliongeza
ya kwamba ukuaji wa benki yake umeenda sambamba na mafanikio
yanayojumuisha tuzo kubwa mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo
Tuzo ya Mlipa Kodi Bora wa Mwaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
iliyopewa kwa miaka miwili mfululizo.
Alibainisha
kuwa ongezeko la thamani ya gawio kwa wanahisa na hata thamani ya hisa
moja moja, vinaakisi uimara, umadhubuti na ubora wa NMB, ambayo mwaka
2019 ilitoa gawi la Sh. Bilioni 33, lililoongezeka hadi kufikia Sh.
Bilioni 181 mwaka huu, huku thamani ya hisa moja ikipanda kutoka 2,300
hadi Sh. 5,440.
Bi
Zaipuna aliishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kuweka miongozo sahihi na mazingira bora,
rafiki na wezeshi ya kutoa huduma za kibenkii nchini kiasi cha
kuharakisha ukuaji kiuchumi kwa taasisi za fedha na kukuza pato la taifa
kwa ujumla.
Sunday, October 13, 2024
NMB yamtambulisha Mtoa Huduma kwa Wateja wa Kidigitali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment