Wednesday, October 09, 2024

TANZANIA NA OMAN KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MUHIMU YA MAENDELEO

  Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia) na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.

Na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
 
Tanzania na Oman zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji, kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya kodi pamoja na kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
 
Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.
 
Mhe. Dkt. Nchemba, alisema kuwa ajenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha inawezesha sekta binafsi kuwa na nguvu, sambamba na uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji, hivyo ushirikiano kati ya nchi hizo utaendelea kunufaisha sekta binafsi na wawekezaji kwa kiasi kikubwa.
 
“Serikali zetu mbili zimeanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja inayosimamia maeneo ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, ikiwemo biashara na uwekezaji, hivyo natarajia kutakuwa na fursa ya kupanua zaidi ushirikiano wetu wa maendeleo kwa manufaa ya watu wetu” alisema Dkt. Nchemba
 
Alikubali maombi ya Balozi wa Oman ambaye alisisitiza umuhimu wan chi yake kujifunza zaidi kuhusu mifumo ya kodi kutoka Tanzania kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ina uzoefu mkubwa katika aneo hilo na kwamba nchi yake imeanza kutoza kodi hivi karibuni. 
 
“Tunatazamia Ushirikiano wa mafunzo hasa kwenye masuala ya kodi, na sehemu ambazo nchi zetu hizi mbili zina utaalamu mahsusi, lengo ni kujengeana uwezo pamoja ili tuweze kunufaika zaidi” alisema Dkt. Nchemba.
 
Naye Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika masuala ya kodi na ameona fursa ya kubadilishana uwezo katika masuala ya kodi ikiwa ni moja ya ajenda kubwa ya ushirikiano kati ya nchi hizo.
 
Mhe. Balozi Al-Shidhani, alisema kuwa biashara kati ya nchi hizi mbili umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kuna tija kubwa ya kuondoa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
 
“Tunapenda kusema kuwa Oman tunataka kujifunza namna ya kushughulikia masuala ya ukusanyaji wa mapato kwa Kuwa Tanzania tayari imepiga hatua katika masuala hayo na sisi tumeanza miaka ya karibuni, kwa hiyo tuna mengi ya kujifunza” alisema balozi huyo.
 
Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria Wizara ya Fedha, Bi. Mwantumu Sultan na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia) na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati) akiongoza kikao chake na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na balozi huyo katik Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili. Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Melckzedeck Mbise (wa pili kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria Wizara ya Fedha, Bi. Mwantumu I. Sultan ( wa kwanza kushoto) na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) akizungumza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al-Shidhani, akizungumza jambo wakati wa kikao na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.
 

Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akipokea zawadi ya Kitabu chenye historia ya Oman, kutoka kwa Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Mhe. Saud Al-Shidhani, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao, yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana kuhusu kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo, katika Sekta ya Nishati na Madini, kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji baina ya nchi hizo, Ushirikiano wa mafunzo katika masuala ya Kodi pamoja na kuondoa Utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji na wafanyabiashara watakaofanya shughuli zao kati ya nchi hizo mbili
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...