EPZA YATOA ELIMU KWA WADAU NA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA

 



Mamlaka ya Uwekezaji EPZA inaendelea kutoa elimu kwa wadau na wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho ya saba ya teknolojia katika sekta ya madini sambamba na kueleza fursa zilizopo za uwekezaji nchini.

Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa Habari, Afisa wa uhamasishaji uwezekezaji wa EPZA Blandina Mwasamwene ameeleza kuwa Mamlaka hiyo inaendeleza juhudi za serikali za kuhakikisha wanachi wanapata fursa ya kupata elimu ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia programu zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo, Mwasamwene amesema wana jukumu la kumuwezesha mwekezaji kupata leseni itakayomwezesha kupata eneo maalum la ujenzi wa kiwanda ili kuuza ndani ya nchi kwa asilimia 20 na nje asilimia 80.

Amefafanua kuwa Mamlaka pia imetenga maeneo ya uwekezaji wa viwanda katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini, ambayo kati ya maeneo hayo yapo yale yaliyoendelezwa kwa kujengwa miundombinu inayomwezesha mwekezaji kufika na kuanza ujenzi wa kiwanda moja kwa moja.

Maeneo hayo ni pamoja na Bagamoyo Pwani, Manyara, Mtwara na Tanga, pamoja na sehemu nyinge nchini, ambayo yapo tayari na mwekezaji apatiwa ili kuanza ujenzi wa kiwanda chake.

Comments