Na Mwandishi Wetu
Baraza la Mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya darasa la saba huku ufaulu wa jumla ukingozeka kwa asilimia 0.29, huku watahiwa 45 walifanya udanganyifu wamefutiwa matokeo yao na 16 waliondika lugha za matusi kwenye karatasi zao za majibu nao wamefutiwa pia matokeo yao kwa mujibu wa sheria
Akizungumza wakati akitangaza matokeo hayo leo Octaba 29,2024 jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa baraza hilo Dkt Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa 974,229 ya watahiniwa wenye matokeo wamefaulu mtihani huo kwa mwaka 2024.
“Kati ya watahiniwa hao 974,229 waliofaulu,wavulana ni 449,057 sawa na asilimia 81.85 na wasichana ni 525,172 sawa na asilimia 80.05 ambapo mwaka 2023 wavulana waliofaulu walikuwa 80.59 na wasichana walikuwa asilimia 80.58”,Amesema Dkt Mohamed.
Aidha amesema kuwa ufaulu wa somo la kiswahili ni mzuri ambapo asilimia 86.58 ya watahiniwa wamefaulu huku somo la kiingereza ukiwa ni asilimia 43.48.
Sambamba na hayo baraza limezuia kutoa matokeo ya wanafunzi 418 ambao waliugua au kupata matatizo mbalimbali na kushindwa kufanya kwa idadi kubwa ya masomo yote.
“Watahiniwa hao ambao matokeo yao yamezuiwa tumewapa furss ya kurudia na kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi(PSLE)mwaka 2025 kwa mujibu wa kifungu cha 32(1)cha kanuni za mitihani”,Amesema.
Akizungumzia kuhusu kufutiwa kwa matokeo kwa waliofanya udandanyifu na wengine kuandika lugha ya matusi kwenye mitihani yao amesema matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa sheria kifungu cha 5(2)(j) cha sheria ya baraza la mitihani sura 107.
Aidha NECTA inazipongeza kamati zote za uendeshaji Mitihani za Mikoa na Halmashauri/Manispaa,wakuu shule,wasimamizi na wasahihishaji wa mtihani huo kwa kazi kubwa na nzuri waliyojfanya katika kutekeleza jukumu la uendeshaji wa mtihani huo.
Matokeo ya Mtihani huo yanapatikana katika tovuti zifuatazo www.necta go.tz
www.moe.go.tz na www.tamisemi.go.tz.
Comments