Friday, September 29, 2017

MTENDAJI MKUU WA TFS, PROF. DOS SANTOS SILAYO AFANYA ZIARA WILAYANI MKURANGA KWA AJILI YA KUIMARISHA UHIFADHI NA KUJADILI MIKAKATI YA KUZUIA WAVAMIZI KWENYE MISITU WA HIFADHI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alimpomtembelea jana Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga ofisini kwake akimuonesha baadhi ya maeneo kwenye ramani jinsi vyanzo vya maji vilivyoharibika kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuvamia kwa kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Misitu. Mwingine ni Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wa Wilaya ya Mkuranga Christina Mohamed
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akiteta neno na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakati wa ziara ya kujionea jinsi wananchi walivyovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Msitu wa Vikindu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo kuu akisaini jana kitabu cha wageni mara alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ikiwa lengo la ziara hiyo ni kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi kwenye msitu wa hifadhi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akimuonesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo baadhi ya maeneo ya Hifadhi yaliyovamiwa na kuanzishwa shughuli za kibinadamu katika Hifadhi ya Msitu wa Vikindu. Lengo la ziara Mtendaji Mkuu wa TFS hiyo ilikuwa ni kuimarisha uhifadhi kwa kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi kwenye msitu wa hifadhi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...