Mpango wa Taifa wa Damu salama kanda ya mashariki Dar es Salaam jana ulikabidhi chupa za Damu 300 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akizungumza wakati wa makabidhiano Afisa uhusino Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Rajab Mwenda alisema chupa hizo za Damu zitasaidia kuokoa maisha ya wahitaji hospitali na zimepatikana kutokana na kampeni ya kukusanya Damu ambayo imeanza wiki hii ambapo mkoa wa Dar es Salaam mpaka jana ulikuwa umeisha kusanya zaidi ya chupa za damu 500.
Bw. Rajab alitumia fursa ya makabidhiano kuwashukuru Jumuiya ya Khoja shia kwa mwitikio wao mkubwa wa kuchangia Damu kwa hiari siku ya Ashura 24/9/2017. Siku ya Ashura ni siku ambayo Jumuiya ya Khoja shia kila mwaka huwa wanaadhimisha kifo cha Imam Hussein kwa kuchangia Damu. Pia alitoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu kama Ishara ya kuunga mkono jitihada za Mpango kuhamasisha jamii kuchangia Damu ili kupunguza vifoo vinavyoweza sababishwa na uhaba wa Damu
Mwakilishi wa Hospitali ya Muhimbili Bw. Hamisi Shabani Kubiga alishukuru Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kugawia Hospitali ya muhimbili kiasi hicho cha chupa za Damu, chupa hizo zitasaidia kutibu kina Mama na watoto wenye uhitaji wa Damu, Majeruhi wa ajali na magonjwa mengine alisema Bw. Hamisi
Comments