Monday, September 25, 2017

Dkt. Harrison Mwakyembe awapongeza JWTZ katika Uhifadhi wa Kumbukumbu za Kitaifa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia baadhi ya picha za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani iliyotumika wakati wa Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia bango linaloelezea kumbukumbu za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia mchanga wa makaburi yaliyofukuliwa ya Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia moja ya silaha za kivita iliyotumiwa na Mashujaa wa Tanzania wakati wa Vita vya Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Na Benedict Liwenga-WHUSM.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.

Pongezi hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo yaliyoweza kuhifadhiwa kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara la Afrika ikiwemo mahitaji ya ziada ya maeneo hayo.

Mhe. Mwakyembe amesema kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika kuyatembelea maeneo hayo ni kujua kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na mashuhuda wa matukio ya kumbukumu za maeneo husika kwa ajili ya kuandika historia ya Afrika kwa ushahidi uliotafutwa na Waafrika wenyewe.

“Tunakipinid kifupi kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo tunazihifadhi, tunaandika historia yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya kuandikiwa na Waliotutawala huko nyuma kwa ushahidi tulioutafuta wenyewe”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa JWTZ imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ya kumbukumbu za kitaifa, jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa ajili ya Mradi wa Ukumbozi wa Bara la Afrika.

“Tumeanza kukubaliana wote katika SADC na katika nchi za Afrika, ni lazima tuingize katika mitaala ya shule zetu hizi harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ili vizazi vijavyo viweze kufahamu mambo haya hususani tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, katika ziara hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa kuongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa kuja na Mpango wa Usajili wa Vizazi vya Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka Mitano ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...