Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, Akizungumza na waandishi wa habari ( Hawapo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam, Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi Milioni 200 zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim ( Hayupo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam.
--
Wadhamini wakuu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom imetangaza kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3 jijini Dar es salaam.
Vodacom imekuwa ikisubiri kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa - Taifa Stars za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha tukio la kukabidhi zawadi hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema katika msimu wa 2012/2013 "Tulikuwa tukisbiri wakati muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu kumalizika kwa ligi mwezi uliopita mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa ari na nguvu timu yetu ya taifa katika kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil." Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Mwalim amesema maandalizi yote ya zoezi hilo yamekamilika kwani hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu baada ya ligi kumalizika zaidi ya timu ya taifa - taifa stars.
Mwalim amesema hafla ya utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji wa vilabu ambao miongoni mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi wa TFF na walimu wa timu ya taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema kuingiza maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.
Mwalim ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la Soka - TFF na kamati ya ligi kwa uvumulivu wao wakati wote ambapo Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka wa kukabidhi zawadi.
"Tendo la kukabidhiwa zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote anaeshinda, tumeona uvumilivu mkubwa na wenzetu walituelewa wakati tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila kuharibu concetratiuon ya taifa. Tumeonesha umoja wetu."
Mbali ya mabingwa timu ya Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia zawadi za wachezaji na wadau wengine mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye maeneo yao.
Vodacom itakabidhi zawadi za fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika nafsi ya pili hadi ya nne.
Wengine watakaonufaika na zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora, mwalimu bora, timu iliyoonyesha nidhamu na mfungaji bora.
Vodacom imekuwa ikiidhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya misimu mitano sasa huku ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya ushindani kadri miaka inavyosonga mbele.
Mwisho.......
No comments:
Post a Comment