Sunday, June 16, 2013

KITITA CHA MILIONI 15 CHAMWAGWA KUDHAMINI SHINDANO LA UREMBO LA REDD`S MISS TANGA 2013!!

3
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya L Hayat Investment Limited ya nchini Oman, imetoa dola za kimarekani 10,000 ni sawa na sh.milioni 15 za kitanzania, kwa ajili ya kudhamini shindano la urembo la redd’s miss Tanga, linalotarajiwa kutimua vumbi Juni 22 kwenye Uwanja wa mkwakwani.
Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, ambaye ndiye muandaaji wa shindano hilo, alisema kuwa, amefurahi kupata kiasi hicho cha fedha kwa kuwa kimemsaidia kwa asilimia kubwa kufanikisha shindano hilo.
Alisema kuwa kwa namna nyingine anamshukuru .mkurugenzi wa kampuni hiyo Shekhe Salim Al Harthy kuweza kumsaidia kiasi hicho. “Namshukuru sana mr Salim kwa. Kuweza kunisaidia kama hivi, nina amini kila kitu kitakuwa kipp sawa”alisema Asha.
Katika hatua nyingine Asha alisema, katika shindano hilo jaji anatarajiwa kuwa mwandishi wa Freemedia inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari Clezencia Tryphone ‘Tasha’ ambaye atasaidia kazi na Miss Tanzania miaka kadhaa iliyopita ambaye yuko katika mazungumzo naye ya mwisho.
Aliwataja warembo hao kuwa ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Wahida Hashimu(20), Tatu Athumani (19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21),Hzina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moreli (21) na Hawa Twaybu(21)
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha na kudai kuwa burudani atazitangaza katikati ya wiki hii.
Redd’s, Miss Tanga, imedhaminiwa na L Hayat Investment Limited, Dodoma Wine, CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers Cloud’s Media Group,  pamoja na Blog Michuzi Media Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...