Edward akiwa wodini Moi
Afisa
Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis
Nkomola amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake
Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.
Edward
Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo
katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15
mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo
Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa
saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali,
walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili
ya harusi yake.
Taarifa
hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo
walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza
kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja
mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha,
simu na vifaa mbali mbali vya harusi.
Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa Elizabeth.
Nkomola
amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa
MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari
kwa ukaribu zaidi.
No comments:
Post a Comment