Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com |
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabidhi tuzo |
Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo |
Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizodhaminiwa na kampuni ya Steps. |
…………………………………………………………………………
KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya
Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu
nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo
hizo
Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa
wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo
iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya
kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo
Baadhi ya washindi ambao
walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela ‘Steve
Nyerere’, Issa Mussa ‘Cloud 112′ Mohamed Nurdini ‘Chek budi’ Nice
Mohamed ‘Mtunisi’ Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike
Wakati katika kinyanganyiro cha
kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Steven ‘JB’ huku msanii
bora wa kike ikienda kwa mwana dada Irene Uwoya
na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda ‘Jimmy Masta’
Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi’ Ray’ na kampuni yake ya RJ Filamu
mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za
heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani
moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko ‘Sajuki’ John Stefano,Hussein
Ramadhani Mkiety,’Sharo Milionea’
Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi
No comments:
Post a Comment