MABAO 4-2 ilitosha kuiondosha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika safari ya kwenda Brazil kwenye mashindano ya Kombe la Dunia,Washambuliaji wa Kimataifa wa Timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, Solom Kalou pamoja na Gervinho waliiwezesha timu yao kuitupa Stars nje ya mashindano hayo.
Stars ndiyo iliyoanza kupata bao la kuongonza kupitia kwa Amri Kiemba akiunganisha mpira nyavuni baada ya mabeki wa Ivory Coast kushindwa kuondoa mpira uliorushwa na Erastal Nyoni.
Wakati watanzania elfu 60 waliokaa kwenye viti vya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakiendelea kushangilia bao hilo,Ivory Coast wakasawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji Traore Lacina.
Thomas Ulimwengu alipachika bao la pili baada ya kuwashinda nguvu mabeki watatu wa Ivory Coast na kuwainua watanzania kwenye vitu vyao, kufungwa kwa bao hilo ilizidi kuwachanganya miamba hao wa soka kutoka Afrika Magaribi.
Mshambuliaji wa Arsenal Gervinho aliweza kutumia uzoefu wake wakujiangusha na kumfanya Mwamuzi wa mchezo huo Mehdi Abid kutoka Algeria kuizawadia Ivory Coast penalti iliyopigwa na Toure iliyomshinda kipa namba moja wa Stars Juma Kasseja na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Ivory Coast waliokuwa wakicheza soka la malengo kutokana na tabia yao ya kufanya mashambulizi makubwa pale wanapofungwa tu walifanikiwa kupachika bao la tatu kupitia kwa Toure aliyepiga mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 na kuitinga wavuni.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Ivory Coast walikuwa mbele kwa mabao 3-2, kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta ushindi, lakini uzoefu wa mshambuliaji Gervinho iliwashinda mabeki wa Stars na kutoa pasi iliyonaswa na Bonny Wilfred nakupachika bao la nne.
No comments:
Post a Comment