Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja Akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na maaskari wa
Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara baada ya kuwasili katika viwanja
hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja akipokea Salam za heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Mbeya
Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la
Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C.
Minja (ambaye haonekani pichani) wakati wa hafla ya kuwatunuku nishani.
Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo
Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za kutunuku nishani
Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja
SACP C. A Keenja akitaja majina 29 ya
Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa Nishani ya Utumishi uliotukukuka
Tanzania, Utumishi Muda Mrefu Tanzania, Utumishi mrefu na tabia njema na
Mwenge wa Uhuru daraja la nne.
Askari Mwanamke akitembea kwa ukakamavu kuelekea eneo linalotumika kutunukia Nishani kwa Maaskari wa Jeshi la Magereza
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya utumishi ulio Tukuka Tanzania
ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema SGT
Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza Kiwira
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya kutunukiwa nishani ya
utumishi mrefu na Tabia njema.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akiwa katika picha ya pamoja na Maaskari 29 waliotunukiwa Nishani mbalimbali
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi
la Magereza wastaafu.
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliotunukiwa Nishani
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akibadilishana jambo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP
John C. Minja akiwa katika picha ya Pamoja na Afisa Habari wa Jeshi la
Magereza Makao Makuu Insp. Lucas Mbonje wakizungumza na waandishi wa
Habari mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya.
**********************
RAISI wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani mbali
mbali Askari 29 kwa Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Nyanda za juu
kusini.
Mbali na Nishani
hizo pia Jeshi hilo limesema limejipanga kuhakikisha linaanza
kujitegemea na kuepukana na Bajeti za Serikali katika kujiendesha
kutokana na uwepo wa Rasilimali nyingi zinazoweza kuzisaidia hususani
Wafungwa na Ardhi kwa ajili ya kuzalisha Chakula.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Kamishina Jenerali wa Magereza Nchini, CGP John C.
Minja wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku Nishani Maaskari wa Jeshi hiyo
iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ruanda Jijini Mbeya.
CGP Minja alisema
Jeshi la Magereza linauwezo wa kujiendesha kutokana na kuwa na
rasilimali na nguvu kazi ambazo zitatumika katika kuzalisha chakula ili
kuepuka kusubili Fedha kutoka Serikalini ambazo huchukua muda mrefu kupatikana na milolongo kuwa mingi.
Aliongeza kuwa
hata baada ya kuanza kujitegemea kwa Jeshi hilo kutawapunguzia gharama
walipa kodi ambao wamekuwa wakikatwa fedha zao kila siku ili kufanikisha
upatikanaji wa Chakula kwa Wafungwa na Shughuli nzima za Jeshi la
Magereza Nchini ikiwemo upungufu wa Majengo.
Kamishina huyo pia
aliiomba Serikali kuunga mkono juhudi hizo na mikakati ya kutaka
kujitegemea ili kuzipunguzia Taasisi Mbali mbali kama Wabunge ambao kila
mara wamekuwa wakijadili suala la uboreshaji wa Jeshi la Magereza
Nchini.
“ Tangu niingie
madarakani lengo langu na ajenda kuu ni kuboresha jeshi la Magereza ili
liweze kujitegemea ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia gharama zisizokuwa za
ulazima kwa wanaokatwa fedha katika vipato vyao” alisema CGP Minja.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Askari 29 walitunukiwa Nishani Kutoka kwa Kamishina
Jenerali wa Magereza ambaye alitumia Mamlaka aliyokasimiwa na Raisi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Kifungu cha 34(4) Cha katiba ya
Jamhuri ya Muungano ya kuwavisha Nishani Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza ambao walitunukiwa Nishani mbali mbali lakini hawakuvishwa na Raisi Aprili 26, Mwaka huu.
SACP Keenja ambaye ndiye alikuwa akitaja majina ya Askari waliotunukiwa Nishani hizo alisema Orodha
ya majina ya Maafisa na Askari pamoja na Nishani zao yameelezwa na
kuainishwa katika Taarifa ya Kawaida na kutangazwa kwenye Gazeti la
Serikali namba 84/2013 la April 26, Mwaka huu.
Alizitaja Nishani
hizo kuwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi uliotukuka ambayo hutunukiwa
Maafisa waliokwenye Utumishi wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambapo kwa
Jeshi la Magereza hutunikiwa wenye Cheo cha Mrakibu au wa juu ya Cheo
hicho waliotumikia jeshi hilo kwa Miaka 20 Mfululizo ambayo alitunukiwa
Askari mmoja ambaye ni ACP Hawa Mollel Simon ambaye pia ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Rukwa.
Nishani ya Pili
hutunukiwa kwa Askari kuanzia Nyota Moja ambao wametimiza utumishi wa
miaka isiyopungua 15 mfululizo akiwa na tabia njema ya kuweza kusifiwa,
Nishani ambayo alitunukiwa Askari mmoja ambaye ni ACP Ally Abdalah
Kaherewa ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma.
Nishani ya Tatu ni
kwa ajili ya askari wenye Cheo cha Wakaguzi, Wakaguzi wasaidizi,
Stesheni Sajini, Sajini na Koplo waliotumikia jeshi la Magereza miaka 15
Mfululizo ambayo huitwa Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzani ambayo
walitunukiwa Askari 18.
SACP Keenja
aliitaja Nishani ya nne waliotunukiwa asakari hao kuwa ni kwa wale
wanajeshi waliohai ambao walizaliwa Disemba 9, 1961 au kabla ya hapo na
mbao wamefanya kazi katika katika Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa muda
wa Miaka 35 au zaidi wakiwa Jeshini wenye sifa na tabia njema ambayo
huitwa Nishani ya Mwenge wa Uhuru daraja la Nne waliyotunukiwa askari 9.
No comments:
Post a Comment