Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa
(Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Morocco
iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoa
kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa maoni ya mchezo huo, Poulsen
alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo alitoa adhabu kali ambayo haiendani na
kanuni za FIFA.
Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundu
baada ya kugongana na Abderazak Hemed Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika
dakika ya 37.
“Hakuwa na
sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Morocco
penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaa
dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi.”
Poulsen
alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana uwanjani
na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kyemba. Morocco walishinda kwa 2-1.
“Kama
tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii lakini
refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama hii,” alisema
Poulsen.
Kocha huyo
alisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama Morocco ni jambo la
kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza
kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapili
ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi ya
Jumapili.
Tanzania
iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6,
Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa Stars
imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na itaendelea na kambi ya
wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha wa
Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa na
walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata
faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha
sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhamini
Taifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa walicheza pungufu
na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika
hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja linaonesha
kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema wao
kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini hii ni
safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita tangu Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager ianze udhamini huo.
No comments:
Post a Comment