Tuesday, June 25, 2013

VOA KUKUTANA NA VIJANA WA MJINI DODOMA KATIKA PROGRAME YA JE NIFANYEJE?


Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika Idhaa ya Kiswahili (VOA) ikishirikiana na USAID limeandaa mkutano mkubwa wa Vijana utakao fanyika kesho mjini Dodoma maarufu kama Je Nifanyeje?.


Washiriki wa mkutano huo ni vijana mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Vijana wengine wa mtaani Dodoma wamealikwa kuhudhuria.

Mtangazaji Mashuhuri  aliyejiunga na idhaa hiyo mwaka 2008 akitokea kituocha ITV na Redio One Sanday Shomari ndiye atakuwa akiongoza mkutano huo.


Wakizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge mjini Dodoma, Sande Shomari pamoja na Bi. Rose Mwakitwange (pichani juu) wamesema maandalizi  ya mkutano huo yamekamilika na mjadala wake utarushwa moja kwa moja na redio Mshirika ABM FM ya mjini Dodoma.


Aidha Bi Rose Mwakitwange ambaye aliwahi kuwa C.E.O wa New Habari Group amewataka wanahabari nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuandishi na wazitumie katika kuelimisha umma na kujipatia kipato zaidi.

Mwakitwange amesema kuwa Wanahabari wana wajibu wa kuisaidia jamii kufahamu vitu vingi vinavyowatatizo hivyo Mwandishi wa Habari akitumia vyema taaluma yake ndiye mtu pekee anaeweza kujibu maswali hayo ya jamii katika nyanja mbalimbali kwa kuandika vitu kwa undani na umakini.

Pia amewataka waanahabari kujitokeza na kujiandikisha ili washiriki Mkutano wa Mafuta na Gesi maana utawawezesha kufahamu masuala mbalimbali na kuwapa mbinu za namna ya kuandika habari zihusuzo gesi na mafuta nchini.

JK AMWAPISHA MWANTUMU MAHIZA KUWA SKAUTI MKUU WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA

  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Skauti 
Mkuu waChama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu
 Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam
 Jumatatu Juni 23, 2013.
 Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania mteule Mhe.
 Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini 
Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na skauti 
kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti 
Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa 
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya
 kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti 
Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea 
kazi Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania 
Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  
Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu
 Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam
 Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  
Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania 
Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha 
 Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu 
Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Jaji Kiongozi Fakih 
Jundu na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania 
Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu
 jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu 
Mahiza pamoja na viongozi wa maskatu na skauti  
baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam 
Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu 
Mahiza na familia yake baada ya kumuapisha  Ikulu
 jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu 
Mahiza pamoja na waheshimiwa wabunge ambao ni 
maskauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini 
Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na skauti 
Ismail Aden Rageh na wabunge maskauti  Ikulu jijini
 Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu 
Mahiza pamoja na wanachama wa UWT wilaya ya Ilala  
baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam 
Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti 
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu
 Mahiza na viongozi wa skauti nchini baada ya 
kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu 
Juni 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na 
skauti Livingstone Lusinde ambaye pia ni 
Mbunge wa Mtera  Ikulu jijini Dar es salaam
 Jumatatu Juni 23, 2013

Monday, June 24, 2013

RAIS KAGAME AFANYA MABADILIKO JESHINI

kagame 7f7aeRais Kagame afanya mabadiliko kwenye uongozi mkuu wa jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Jenerali Patrick Nyamvumba amechukua nafasi ya jenerali Charles Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002.
Mkuu mpya wa majeshi ya Rwanda,alikuwa kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2009.
Mabadiliko hayo pia yameshuhudia wadhifa mpya katika uongozi wa jeshi la Rwanda, ambao ni wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi uliopewa Brigedia jenerali Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo na kuwa meja jenerali.Jack Nziza amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu katika wizara ya ulinzi.Pia mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje kanali Dany Munyuza ameteuliwa kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya Rwanda.Sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi. Chanzo: bbcswahili

Waziri Membe apokea hati za utambulisho wa mabalozi


 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation this morning received copies of Credentials from the Designate Ambassador T. Raveenthiran of Sri Lanka to the United Republic of Tanzania with offices in Nairobi, Kenya.
 Hon. Membe in a discussion with Designate Ambassador Raveenthiran (center) of Sri Lanka and a Senior Officer in the Sri Lanka Embassy during their meeting in Dar es Salaam this morning. 
Hon. Minister Membe explains something during his discussion with Designate Ambassador Raveenthiran of Sri Lanka in his office in Dar es Salaam.
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation receiving copies of Credentials from Designate Ambassador Ittiporn Boonpracong of Thailand to the United Republic of Tanzania with offices in Nairobi, Kenya.
 Hon. Bernard K. Membe in a discussion with Designate Ambassador Ittiporn Boonpracong of Thailand.  Also in the photo is Mr. Omary Mjenga, Assistant Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation and Ms. Sudkanueng Nivestratana, Second Secretary in the Royal Thai Embassy.
Hon. Bernard K. Membe (MP), explaining something during his discussion with Designate Ambassador Ittiporn Boonpracong of Thailand during their meeting this morning in Dar es Salaam.
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation receives copies of Credence from Designate Ambassador Shesudin Ahmed Roble of Ethiopia to the United Republic of Tanzania with offices in Nairobi, Kenya.  The ceremony took place earlier today in the Minister's office in Dar es Salaam.
 Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation thanks Designate Ambassador Roble of Ethiopia at the end of their meeting earlier today in Dar es Salaam.
 Hon. Bernard K. Membe (MP) (right), listening carefully to Designate Ambassador Shesudin Ahmed Roble during their meeting earlier today.
Hon. Minister Membe in a candid moment with Designate Ambassador Roble of Ethiopia and his Embassy Counsellor Eskindir Y. Asfaw. All photos by Tagie Daisy Mwakawago-Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation

PRESS BRIEFING BY DEPUTY NATIONAL SECURITY ADVISOR BEN RHODES, SENIOR DIRECTOR FOR AFRICAN AFFAIRS GRANT HARRIS, AND SENIOR DIRECTOR FOR DEVELOPMENT AND DEMOCRACY GAYLE SMITH ON THE PRESIDENT’S UPCOMING TRIP TO SENEGAL, SOUTH AFRICA AND TANZANIA

THE WHITE HOUSE | Office of the Press Secretary | June 21, 2013

Hotuba ya Profesa Issa Shivji '' Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu Ya Katiba Mpya'' Aliyoitoa katika mhadhara wa kuaga Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliyofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam


Profesa Issa Shivji
--

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ashiriki Sherehe Za Kuwaaga viongozi na watumishi waliohama na wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Tamisemi, Makatibu Tawala wa Mikoa


 Makatibu Tawala wa Mikoa Wastaafu, Bernard Nzungu  (kushoto) na Getrude Chipaka wakisakata Rhumba katika sherehe ya kuwaaga viongozi na watumishi waliohama na wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka ya serikali za mitaa iliyofanyika kwenye viwanja vya Buge Mjini Dodoma Juni 22, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi runinga ya nchi 32 Katibu Twala wa mkoa wa Pwani Mstaafu, Bernard Nzungu katika sherehe ya kuwaaga viongozi na watumishi waliohama na wastaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka ya serikali za mitaa iliyofanyika kwenye viwanja vyaBuge Mjini Dodoma Juni 22, 2013. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Vodacom kukabidhi zawadi ligi kuu Julai 3

  Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, Akizungumza na waandishi wa habari    ( Hawapo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam,  Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi Milioni 200 zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim ( Hayupo pichani)  Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam.
-- 
Wadhamini wakuu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom imetangaza kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3 jijini Dar es salaam.

Vodacom imekuwa ikisubiri kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa - Taifa Stars za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha tukio la kukabidhi zawadi hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema katika msimu wa 2012/2013 "Tulikuwa tukisbiri wakati muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu kumalizika kwa ligi mwezi uliopita mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa ari na nguvu timu yetu ya taifa katika kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil." Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

Mwalim amesema  maandalizi yote ya zoezi hilo yamekamilika kwani hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu baada ya ligi kumalizika zaidi ya timu ya taifa - taifa stars.

Mwalim amesema hafla ya utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji wa vilabu ambao miongoni mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi wa TFF na walimu wa timu ya taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema kuingiza maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.

Mwalim ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la Soka - TFF na kamati ya ligi kwa uvumulivu wao wakati wote ambapo Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka wa kukabidhi zawadi.

"Tendo la kukabidhiwa zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote anaeshinda, tumeona uvumilivu mkubwa na wenzetu walituelewa wakati tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila kuharibu concetratiuon ya taifa. Tumeonesha umoja wetu."

Mbali ya mabingwa timu ya Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia zawadi za wachezaji na wadau wengine mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye maeneo yao.

Vodacom itakabidhi zawadi za fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni  kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika nafsi ya pili hadi ya nne.

Wengine watakaonufaika na zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora, mwalimu bora, timu iliyoonyesha nidhamu na mfungaji bora.

Vodacom imekuwa ikiidhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya misimu mitano sasa huku ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya ushindani kadri miaka inavyosonga mbele.

 Mwisho.......

Taarifa Maalum Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Juu ya Kufungwa Kwa Sehemu ya Barabara ya Kontena, Kanisani-Msikitini hadi Changanyikeni

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
OFFICE OF THE DEPUTY VICE-CHANCELLOR
(ADMINISTRATION)
P.O. BOX 35091 - DAR ES SALAAM - TANZANIA 
.
Tel.:    022 2410500 - 8 Ext.
2003
 
           022 2410394 - Direct Line
Fax:    022 2410718
Ref:     z1/18
Telegram:  University of Dar es Salaam
E-mail:    dvc-pfa@admin.udsm.ac.tz
Website:   www.udsm.ac.tz 
21  Juni, 2013   
Wanajumuiya Wote

YAH: KUFUNGWA KWA SEHEMU YA BARABARA YA KONTENA—KANISANI/MSIKITINI— CHANGANYIKENI  

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unautaarifu umma kuwa kipande cha barabara kuanzia kumbi za mihadhara ya Yombo 1&2 na Bweni Na. 6 hadi barabara ya Changanyikeni kitafungwa kuanzia Jumapili tarehe 23 Juni 2013.

Barabara inayoanzia kituo cha daladala cha Kontena hadi Bweni Na. 6 ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya ndani ya Chuo tu, ingawa kwa siku za karibuni matumizi ya barabara hiyo yameongezeka kiasi cha kuhatarisha usalama wa wanafunzi na wafanyakazi wanaotumia kumbi za mihadhara na ofisi zilizopo maeneo hayo.

Kwa hiyo, watu wote waliozoea kutumia barabara hiyo kuelekea Changanyikeni kwa vyombo vya usafiri vya moto, wanashauriwa kutumia barabara ya kawaida inayoanzia au kutokea karibu na tawi la NBC.

Tunawapa pole kwa usumbufu utakaojitokeza kwa kufungwa kwa barabara hiyo.

Prof. Y. D. Mgaya
NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO - UTAWALA

Azimo la Mazingira bora na salama kwa waandishi wa habari wakiwa kazini lazinduliwa leo jijini Dar es Salaam

IMG_2565
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamko la Mount Meru la kuwalinda waandishi wa habari wakiwa kazini Afrika Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akizungumza machache wakati wa uzinduzi huo ambapo alisisitiza umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera (wa tatu kushoto), Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge (kushoto). 
IMG_2504
Mtangazaji wa Radio Clouds Fm Regina Mwalekwa akisoma Tamko rasmi la Mount Meru lililoandaliwa siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yaliyofanyika Mei 3-4 mwaka huu jijini Arusha yaliyohudhuriwa na washiriki mbalimbali toka vyombo vya habari, redio za jamii, jumuiya mbalimbali za Kimataifa, Taasisi za mafunzo ya tasnia ya habari na mifuko ya Maendeleo ya Tasnia ya habari kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.
IMG_2519
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla (wa pili kulia) akizundua rasmi Tamko la Mount Meru linalozunngumzia vipengele mbalimbali vitakavyowalinda waandishi wa habari Afrika Mashariki.
IMG_2533
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akionyesha Tamko rasmi la Mount Meru la kutetea Uhuru wa Vyombo vya Habari kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
IMG_2543
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akizindua rasmi CD ya wimbo ulioimbwa na Mjomba Band unaoitwa "Uhuru Wangu" uliopigwa kwa mara ya kwanza wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera ( wa pili kushoto), Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa (kulia) na Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan (kushoto).
IMG_2550
Sasa umezinduliwa rasmi....Kaa tayari kuusikiliza katika radio mbalimbali na mitandao ya kijamii hapa nchini.
IMG_2490
Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa akizungumza umuhimu wa waandishi wa habari kujali maslahi mapana ya taaluma ya uandishi wa habari katika mchakato wa kuandika Katiba mpya kupitia mabaraza ya Katiba ya Wilaya.Vile vile alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika kujadili rasimu ya Katiba mpya iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ili kuhakikisha Taifa linapata Katiba Mpya inayojali Uhuru wa vyombo vya Habari hapa nchini.
IMG_2595
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan akifafanua jinsi Mfuko wa Mwangosi utakavyokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
IMG_2497
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji akiteta jambo na Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) (Wa pili kushoto) na Bi. Rose Mwalimu kutoka UNESCO (wa pili kulia).
IMG_2585
Mdau kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) akitoa maoni yake juu ya tamko la Mount Meru kwenye uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar katika Hoteli ya Peacock.
IMG_2575
Baadhi ya waandishi wa habari waandamizi nchini kutoka kushoto ni Shermax Ngehemera Mhariri wa The African, Hamis Mzee wa MCT .
IMG_2495
Wadau mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari waliohudhuria uzinduzi wa tamko la Mount Meru.
--
Kufuatia Mkutano wa Wadau wa Habari Afrika Mashariki waliadhimia yafuatayo;-

1.Serikali zote nchi za Afrika Mashariki zihakikishe kuwa Katiba za nchi zao zinakuwa na vipengele kwa ajili ya:

-Kuwa na tasnia ya habari ambayo ipo huru, salama na yenye kujitegemea ikijumuisha usalama wa wanahabari.

-Sheria nyingine zote ziheshimu Katiba za nchi zikiendana na vyombo na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.

2. Wamiliki wa vyombo vya habari wafanye marekebisho ya miundo ambayo itazingatia yafuatayo;
- Uendeshaji bira- Ikiwa ni pamoja na masuala ya Ajira, Mishahara, Mikataba, Motisha na Marupurupu mengine ya kifedha.

- Viendeshwe kwa kufuata na kuheshimu miiko ya Kitaaluma.
-Kuhakikisha kuwa wanahabari wote wanakuwa na Bima.
-Vyumba vya habari viongeze uwekezaji katika mitandao ya kijamii pamoja na utoajji elimu kwa wanahabari kuhusu mitandao binafsi yaani Blogs.

3. Baraza la Habari lishirikiane na taasisi na vyama vya kitaaluma vya wanahabari ili kudumisha na kulinda ueledi na umoja katika tasnia ya habari.

4. Wanahabari waanzishe vyama vya wafanyakazi ili kuwezesha na kuongeza mapatano na makubaliano ya hiari sehemu za kazi.

5. Wamiliki wa vyombo vya habari walinde na kutetea usalama wa wanahabari na vyombo vyao kupitia

-Wamiliki wa vyombo vya habari kuweka na kuzingatia taratibu za usalama sehemu za kazi
-Wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanwapatia waandishi wa habari vifaa vya usalama au vya kujikingia na hatari na wawezeshe mafunzo juu ya taratibu za usalama.

-Kujumuisha mitaala ya mafunzo ya usalama na ulinzi katika taasisi zote za mafunzo ya uandishi wa habari.

- Wanahabari wao binafsi wachukue vipaumbele na tahadhari katika usalama wao binafsi.
6. Jumuiya ya Afrika Mashariki lizitake nchi wanachama wake ambao walitia sahihi itifaki ya Udhibiti wa Tovuti wajiondoe katika Mkataba huo ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha utawala bora na uwajibikaji.

7. Serikali za Afrika Mashariki zifanya juhudi katika kuwezesha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria wa kuruhusu uendeshaji bora wa mitandao ya kijamii na wakati huo huo wakilinda uhuru wa wadhibiti ili kuboresha na kuendeleza uhuru wa mitandao ya kijamii katika eneo la Afrika Mashariki.

Saturday, June 22, 2013

YALIOJILI KWENYE KILI TOUR DODOMA LEO HII

 LINEX kwa stage
  Roma Mkatoliki
 Dula na Zebwela kwenye stage walisimamia show
Wapenzi wa burudani Dodoma wakiingia katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa wingi sana.


WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...