Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
akifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba 48 za
kuuza za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala Mchikichini, Dar es
Salaam jana.Anayeongoza kupiga makofi kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC,
Nehemia Mchechu.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akizindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za
Makazi za NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam kwa kuweka jiwe la
msingi katika katika mojawapo ya majengo ya majengo hayo ikiwa ni
mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) , baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.Msondo Ngoma walikuwapo kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Mchikichini
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akizungumza na MC maarufu nchini na Mtangazaji wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba, Ephraim Kibonde (picha ya juu) pamoja na mtangazaji wa TBC (picha ya chini) baada ya uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi za NHC Mchikichini Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka hamsini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , baada ya uwekaji wa jiwe la msingi alikagua ujenzi wa mradi huo wa nyumba.
No comments:
Post a Comment