Gari ya Marehemu Sharo Milionea kama linavyooneka mara baada ya Ajali iliyopekea kupoteza uhai wake!
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga na kushirikiana na wasamalia wema wamewatia mbaroni vijana wanne wanadaiwa kumpora vitu mbalimbali marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali mbaya mwanzoni mwa wiki hii.
Habari za kuaminika toka Mkoani humo zinasema kuwa vijana hao wamekamatwa baada ya kazi nzuri iliyofanbywa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kushirikiana na wasamalia wema ambapo hadi sasa vijana hao wako chini ya ulinzi mkali huku wengine wakiwa bado wanatafutwa.
Habari
zaidi zilisema kuwa vijana hao wamekamatwa jana usiku na waliokamatwa
wamefahamika kwa jina ya Issa Makunera,Farid Hassani,Rashidi
Ayubu,Rashid Makunera na imeelezwa watuhumiwa hao wamekutwa na mali
mbalimbali za marehemu.
Chanzo
chetu toka mkoani humo zilisema watuhumiwa hao pamoja na mali hizo
zimekamatwa katika eneo linanaloitwa Songa Kibaoni na vitu hivyo ni SPEA
TAILI,REDIO YA GARI,BETERI YA GARI,SAA YA MKONONI SURUALI AINA YA JINS
PAMOJA TISHETI ,BEGI PAMOJA NA SIMU YA MKONONI.
No comments:
Post a Comment