Rais Jakaya Mrisho Kikwete amejiuzulu
nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa mujibu wa Katiba ya
chama hicho kupisha uchaguzi kufanyika upya.
Licha ya kujiuzulu lakini Rais Kikwete
anataraji kuchaguliwa tena kwa kishindo kwani ndiye mgombea pekee wa nafasi
hiyo ya Uenyekiti.
Kufuatia kujiuzulu huko nafasi ya
Uenyekiti imeshikiliwa kwa muda na Rais Mstaafu, Benjamini William Mkapa aliyeungwa
mkono na wajumbe wote baada ya jina lake kupendekezwa na Mwenyekiti aliyemaliza
muda wake.
Mbali na Mywenyerkiti pia Sekretarieti
yote ya chama hicho imejiuzulu na inasubiri kuchaguliwa tena baada ya uchaguzi
kukamilika.
Kamanda wa UVCCM
Mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri akiwa na viongozi wa UVCCM Iringa.
Wajumbe wa CCM
kutoka mkoa wa Arusha wakiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa
wakifuatilia matukio ya kampeni ndani ya ukumbi wa Kizota wakati kampeni za
wagombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti bara na visiwani zikiendelea.
Wajumbe wa Mkoa wa
Iringa wakjifuatilia kwa umakini kampebni hizo, ambazo zilikuwa zikifanywa na
Yusufu Makamba na Vuai Vuai kwaajili ya mgombea wa Uenyekiti.
Nchimbi akiwa na
wajumbe wenzake mkutanoni hapo.
Wajumbe wa CCM
kutoka mkoa wa Arusha
wakifuatilia matukio ya kampeni ndani ya ukumbi wa Kizota wakati kampeni za
wagombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti bara na visiwani zikiendelea.
Wanachama wa CCM,
kundi la Diaspora wakipiga picha na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi
mbalimbali wa CCM Taifa.
Wanachama wa CCM,
kundi la Vyuo Vikuu wakipiga picha na Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi
mbalimbali wa CCM Taifa.
Vijana wa Chuo kikuu ambao ni makada wa CCM wakiwa pamoja
Wajumbe kutoka Mwanza wakimsikiliza Mzee Yusuf Makamba akimnadi Jakaya Kikwete.
Wajumbe kutoka Kagera wakifuatilia kampeni. Picha zote kwa hisani ya FATHER KIDEVU
No comments:
Post a Comment