Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo
huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo,
ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini
Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki
(kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
waziri
Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi
Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof.
Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania
nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na
Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi
wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto
za maendeleo.
Mawaziri
Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia) na Salim Ahmed
Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.
Rais
Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo
Mbeki, (Kulia), akimtania Waziri Mkuu Mstaafu na mwenyekiti wa Tume ya
mabadiliko ya katiba ya Tanzania, Joseph Warioba, wakati marafiki hao
walipokutana
kwenye majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika.
Waalikwa mbalimbali wakiwa katika chumba cha majadiliano.
Naibu
waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba,
akichangia mada katika majadiliano hayo ya Duara. Makamba alizungumzia
sana kuhusu masulala ya uchumi.
Mmoja wa waalikwa akichangia mada
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Felix Mosha akizungumza.
Meza
kuu ikifuatilia kwa ukaribu majadiliano hayo. kutoka kushoto ni Rais
Mstaafu wa afrika Kusini, Thabo Mbeki, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
UONGOZI, Prof. Joseph Semboja na Mdhamini wa taasisi ya Thabo Mbeki,
Gloria.
Arnod Kileo nae akichangia mada, kulia ni Prof. Toli Mbwete, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, ni ofisa kutoka Bank M.
Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo
ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.Kulia ni Mgeni Rasmi,
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.
Waziri
wa mambo ya Nje, Bernard Membe (kulia), waziri Makuu Mstaafu, Cleopa
Msuya na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki wakifuatilia Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrikajijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waalikwa wakiwemo wahariri wa vyombo vya habari walihudhuria
majadiliano hayo. kushoto ni Gabi Mgaya kutoka Daily News.
Mwongozaji wa Majadiano hayo, Sauda Simba Kilumanga akisema jambo muda mfupi kabla ya kufunga.
Rais
Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki akizungumza jambo na Waziri Mkuu
Mstaafu, na Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Sinde Warioba huku Katikati waziri wa Mambo ya nje na Ushirikaino wa
Kimataifa, Bernard Membe akichangia wakati viongozi hao wakitoka katika Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrikayaliyoandaliwa na Taasisi ya UONGOZI jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment