Tuesday, November 06, 2012

Bodi ya Korosho yatangaza bei ya korosho msimu huu

  
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania, Mudhihiri Mudhihiri (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu  bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na  960 kwa daraja la pili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Korosho Tanzania, Theofora Nyoni.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano baina yao na bodi ya korosho uliofanyika leo katika ofisi za bodi hiyo jijini Dar es Salaam wakijitahidi kupata matukio muhimu ya mkutano huo. Katika mkutano huo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania, Mudhihil Mudhihili (hayupo pichani) alisema kuwa  bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu
wa mwaka 2012/2013 ni shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na  960 kwa daraja la pili.

   Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihil Mudhihili (kulia) akiwaandikia waandishi wa habari  jina
lake wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo mambo mbalimbali yaliongelewa ikiwa ni pamoja na bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na  960 kwa daraja la  pili.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo.)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...