Wednesday, November 07, 2012

MAKAMU WA RAIS AMJULIA HALI KATIBU MKUU WA MUFTI WA ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI

 
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (wa tatu kulia) wakati akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Katibu Mkuu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga aliyemwagiwa tindikali jana huko visiwani Zanzibar.

Makamu wa Rais akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kumjulia hali Sheikh Soraga.
 
 
...Akiingia kwenye gari tayari kwa safari.
 
Mwandishi wa Habari wa Mheshimiwa Bilal, John Mapinduzi akilifuata gari tayari kuondoka eneo hilo.
 
Mwanausalama akihakikisha kiongozi huyo anaondoka kwa usalama hospitalini hapo.(PICHA HABARI NA HARUNI SANCHAWA GPL-
--
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam kumjulia hali Katibu Mkuu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga aliyenusurika kifo baada ya kumwagiwa tindikali jana huko visiwani Zanzibar.

Kufuatia tukio hilo, amesema kuwa kitendo alichofanyiwa Sheikh huyo ni cha kinyama na hakitavumiliwa na kwamba serikali inafanya juu chini kuwabaini waliohusika na tukio hilo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.“Hatutavumilia kitendo hicho hata kidogo kwa sababu huu siyo utamaduni wetu tuliojiwekea,” alisema Makamu wa Rais.Jana, Rais Jakaya Kikwete alifika hospitalini hapo kumjulia hali Sheikh Soraga.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...