Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara. Amezindua nyumba hizo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 20, 2024, katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi, Naibu Waziri wa Madini Steven Kiruswa, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamisi, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi John Mongela na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara Peter Toima.
Muonekano wa nyumba ambazo zimejengwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua nyumba hizo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 20, 2024, katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabdhi Hati ya nyumba na Biko la geri Agatha Yai ambaye ni muathirika wa maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang. Mheshimiwa Majaliwa uzinduzi wa nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara. Amezindua nyumba hizo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 20, 2024, katika kitongoji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabdhi Hati ya nyumba Innocent Kamili ambaye ni muathirika wa maporomoko ya tope kutoka Mlima Hanang. Mheshimiwa Majaliwa amezindua nyumba 109 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara. Amezindua nyumba hizo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 20, 2024, katika kitongoji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
Comments