Viongozi
na Watendaji wa CCM Kata ya Mwananyamala Wilaya Kinondoni Mkoa wa Dar
es saalam kwa kushirikiana na CCM Mkoa wa Magharib Zanzibar wakiwa
katika ziara ya kukagua na kutembelea mradi wa Reli ya SGR kwa kupanda
reli hiyo kutoka Dar es saalam hadi Morogoro leo tarehe 14/12/2024.
Na Is-haka Omar,Morogoro.
UONGOZI
wa CCM Kata ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam,
kwa kushirikiana na uongozi wa CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar,
wamempongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kutekeleza miradi mbalimbali ya
kimkakati, hasa mradi wa Treni ya SGR (Standard Gauge Railway), ambao
umeleta suluhu kubwa kwa changamoto za usafiri wa nchi kavu nchini.
Pongezi
hizo zimetolewa na viongozi na wanachama wa CCM kutoka Kata ya
Mwananyamala na CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar walioshiriki katika ziara
ya kutembelea mradi huo.
Ziara
hiyo ilianza kwa kupanda treni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro,
ambapo viongozi hao walielezea kutambua na kuthamini juhudi hizo za
Serikali, wakikiri kuwa mradi wa SGR umeleta mabadiliko makubwa katika
sekta ya usafiri nchini.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Katibu wa Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM
Mkoa wa Magharibi Zanzibar, Bi. Msekwa Mohamed Ali, alisema kuwa kupitia
ziara hiyo wamejionea kazi kubwa na nzuri iliyofanywa katika mradi wa
kimkakati wa SGR, akisisitiza kuwa mradi huo umeonyesha matumizi sahihi
ya fedha za walipa kodi.
Aliwataka
wananchi kumpongeza Rais Samia kwa juhudi hizo na kuendelea kumunga
mkono kwa kusafiri na treni hiyo katika safari mbalimbali, ili wawe
mashuhuda wa mafanikio hayo.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mwananyamala, Pili Muongela, alisema kuwa
lengo la ziara hiyo ni kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi
wake kwa kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2020-2025, hasa mradi wa SGR, ambao umekuwa mwarobaini wa kumaliza
tatizo la usafiri nchini.
Akitoa
ufafanuzi wa ziara hiyo, Katibu wa CCM Kata ya Mwananyamala, Stanly
Rufini Mvungi, alisema kuwa ziara hiyo pia ilihusisha kutembelea miradi
mingine, ikiwemo sekta ya utalii kupitia Mradi wa Royal Tour, ambapo
walifanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Mikumi, mkoani Morogoro, na
kujionea wanyama pori na vivutio mbalimbali.
Alisisitiza
kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuthamini mafanikio ya miradi mikubwa ya
kimkakati, kama vile Mradi wa Bwawa la Mwl. Nyerere, ambao umeleta
manufaa makubwa kwa wananchi.
Ziara
hiyo iliwashirikisha viongozi mbalimbali wa chama na jumuiya zake
kutoka Tanzania Bara na visiwani, na ililenga kuonyesha mafanikio ya
Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha
miundombinu ya taifa.
Viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment