AJALI YA GARI YAUA WATU SITA NYASA,WAMO WALIMU WANNE
Watu sita wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma
Ajali
hiyo imetokea leo, tarehe 28 Desemba 2024, wakati wa safari kutoka
kijiji cha Lumalu kilichopo katika Kata ya Upolo kuelekea makao makuu ya
wilaya.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mheshimiwa Peres Magiri,
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambayo imesababisha vifo vya
wafanyakazi wanne wa Serikali, wakiwa ni walimu wa Shule ya Msingi
Lumalu.
Watu wawili wengine, wakiwemo dereva wa gari hilo na raia mmoja, pia amepoteza maisha.
Gari
lililohusika katika ajali hiyo ni la aina ya Prado T 647 CVR, mali ya
Vincent Alel Milinga kutoka kijiji cha Lumalu, Kata ya Upolo, Wilaya ya
Nyasa.
Walimu
waliopoteza maisha ni Damas Damasi Nambombe (Mwalimu),Domenica Abeat
Ndau (Mwalimu),Judith Joseph Nyoni (Mwalimu),na John Silvester Mtuhi
(Mwalimu).
Raia mwingine aliyefariki duni ni Boniface Bosco Mapunda pamoja na dereva wa gari hilo ambaye ni Vincent Alel Milinga.
Comments