Friday, December 20, 2024

SERIKALI YAIPONGEZA WIZARA YA ARDHI KWA UPIMAJI VIWANJA 268 KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG

 








Babati - Manyara 

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) ameipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuhakikisha upimaji wa eneo la kitongoji cha Waret kwa kuzingatia kanuni za mipango miji kwa ajili ya uanzishaji wa makazi kwa waathirika wa maporomoko ya tope.

Mhe. Waziri Mkuu amesema hayo leo Tarehe 20 Desemba 2024 katika uzinduzi wa Nyumba 109 za waathirika wa maporomoko ya tope  yaliyotokea December 03, 2023 zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, kijiji cha Gidagamowd, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. 

Ujenzi wa nyumba hizo ulitokana na maamuzi ya Rais Dkt. Samia baada ya kutembelea eneo hilo ambapo Serikali imesema uamuzi huo ni muendelezo wa dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwalinda Wananchi wake na kurejesha hali ili waendelee na mfumo wa maisha baada ya maafa.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang waratibu zoezi la ugawaji wa viwanja vya ziada vilivyopo katika eneo hilo ili kuendeleza eneo hilo. 

“Tunataka eneo hili lisitambuliwe kama makazi ya waathirika, bali kijiji rasmi chenye huduma zote muhimu za kijamii na liwe kielelezo cha maboresho ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wote.”

Wizara ya Ardhi ilipewa jukumu la kupima, kupanga na kumilikisha eneo la ekari 100 ambapo jumla ya viwanja 268 vilipatikana ikiwa 234 ni makazi pekee, 17 Makazi na biashara, 7 Biashara pekee na 10 huduma za Jamii.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...