Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiagana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli baada ya kuhutubia alipotembelea na kuongea na wakaazi wa Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akinyanyuka juu baada ya kupongezwa kwa utendaji wake bora na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi wa Magomeni Kota wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuelekea katika eneo la makazi ya Magomeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akiongozana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi kuelekea katika eneo la makazi ya Magomeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akitia saini kwenye kitabu cha wageni huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi wakishuhudia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota.
“Wapangaji wote lazima walipe madeni yao, natoa agizo leo wapangaji wote serikalini wanaodaiwa na NHC ndani ya siku saba wawe wameshalipa madeni yao, ” amesema.
Ameongeza kuwa “Wasipolipa endeleeni kuwatolea vitu vyao nje kama mlivyotoa vya jamaa, awe wa UKAWA toa nje, wa CCM toa. “
No comments:
Post a Comment