Sunday, September 18, 2016

BENKI YA CBA YAJA NA HUDUMA ZA KISASA ZA KIBENKI


Mwenyekiti wa Tanzania CEO Roundtable, Ali Mufuruki akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Dk. Gift Shoko wakati wa uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ jijini Dar Es Salaam hivi karibuni. Mufuruki alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana.  Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA Tanzania, Dk Gift Shoko akizungumza na wateja mashuhuri wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ uliofanyika jinni Dar es Salaam hivi karibuni. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.  Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa CEO Round Table nchini, Ali Mufuruki akizungumza na wateja mashuhuri wa benki ya CBA Tanzania katika uzinduzi wa huduma ya ‘Private Banking’ uliofanyika jinni Dar es Salaam hivi karibuni. Kufuatia uzinduzi wa huduma hiyo ya ‘Private Banking’, sasa wateja wa benki ya CBA watapata huduma za kipekee na murua zenye kuwawezesha kufanya miamala kwa ufanisi, haraka na mazingira mwanana.    Wageni waalikwa. 

Benki ya CBA yaja na huduma za kisasa za kibenki Katika mkakati wake wa kuendelea kuboresha huduma zake nchini,Benki ya CBA imezindua huduma mpya kwa wateja wake binafsi zitakazowawezesha kupata huduma za kibenki kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kupata huduma za kibenki kimtandao kupitia simu zao za mkononi. Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya,Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania,Dk.Gift Shoko,alisema kuwa huduma hizi zimelenga kuwarahisishia maisha wateja na kuwawezesha kupata huduma za kibenki kulingana na matakwa yao na kwenda sambamba na mtindo wa maisha wanaoishi.

 Alisema pia wateja wa CBA Tanzania kuanzia sasa wanaweza kutumia kadi za kimataifa za kufanya mihamala ya malipo za Visa Platinum Debit Card na Visa Gold Credit Card kwa fedha za kitanzania na Dola za Kimarekani ambazo zinawawezesha kupata huduma mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa JKIA kwenye sehemu ya kupita watu maarufu (VIP lounge).Alisema huduma hii itawawezesha wateja wa kundi hili kufanya mihamala wakiwa katika viwanja vya ndege 600 kwenye nchi 1,000 na miji mikubwa ipatayo 300 duniani kote.

 “Tunazidi kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja ili wazipate popote na kwa wakati wowote watakapokuwa bila kupoteza muda kama ilivyokuwa hapo awali”.Alisema. Kitengo cha kuhudumia wateja watakaojiunga na huduma hii kwa kuanzia itapatikana jijini Dar es Salaam katika matawi yaliyopo kwenye mitaa ya Ohio na Samora vilevile katika tawi la Arusha. Benki ya CBA Tanzania ambayo ni moja ya Benki kubwa zinazoongoza kwa ubunifu wa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wake ,moja ya huduma ambayo imeianzisha na kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya makazi ya kutoa mikopo ya nyumba inayolipwa hadi kufikia kipindi cha miaka 20. 

 Benki ya CBA Tanzania hadi kufikia sasa inayo matawi 11 nchini kote ambapo 5 yapo jijini Dar es Salaam na mengine katika miji ya Mbeya, Tunduma, Mtwara, Moshi, Mwanza, na Arusha.Pia benki ipo katika nchi nyingine za Afrika Mashariki za Kenya,Uganda na Rwanda ambazo ziko chini ya mwamvuli wa CBA GROUP.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...