#RIPJenistaMhagama #Tanzania #Ruvuma #Uongozi
Dodoma – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema taifa limepata pengo kubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho na kiongozi mashuhuri wa muda mrefu, marehemu Jenista Mhagama.
Akitoa salamu za rambirambi nyumbani kwa familia ya marehemu katika eneo la Itega jijini Dodoma, Makamu wa Rais amesema Jenista Mhagama alikuwa kiongozi shupavu, mwenye heshima na mchango mkubwa katika utumishi wa umma, si tu kama Mbunge wa Peramiho bali pia kama mtendaji aliyeisimamia kwa karibu maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma na majukumu mbalimbali ya kitaifa.
Amesisitiza kuwa marehemu Mhagama alitoa mchango mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika nafasi zote alizowahi kushika, akionesha uadilifu, nidhamu na uzalendo uliotukuka.
Makamu wa Rais ametumia fursa hiyo kufikisha pole kwa familia, ndugu na waombolezaji wote, akiwaombea faraja na ujasiri wa kuendelea mbele katika kipindi hiki kigumu. Amesema kifo ni sehemu ya safari ya mwanadamu, lakini alama na mchango wa marehemu Mhagama vitaendelea kukumbukwa.










No comments:
Post a Comment