Monday, September 12, 2016

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za janga la tetemeko la ardhi lililotokea jana tarehe 10/09/2016 katika Mkoa wa Kagera na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza na Shinyanga.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kufuatia vifo vilivyotokana na tetemeko hilo.

Katika salamu zake Ndg Kinana amesema Chama cha Mapinduzi kinatoa pole kwa wahanga na kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika janga hilo.

Chama cha Mapinduzi kipo pamoja na wahanga, kushirikiana nao kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu pema peponi.

Amina.

Imetolewa na:-

CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)

MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Tarehe 11/09/2016.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...