Tuesday, September 20, 2016

AZAM WAZINDUA PROMOSHEN YA FULL DOWZY KUTWA MARA TATU


Mkuu wa uwendeshaji wa Azam Media, Yahya Mahamedi, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akitangaza huduma mpya ya Full Dowzy kutwa mara tatu (kulia) ni Ofisa habari na Mawasiliano ya nje Azam media, Irada Mtonga. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KITUO cha Azam Tv yazindua Promosheni mpya ya 'Full Dowzy kutwa mara tatu'  ambapo mteja mpya atapewa king'amuzi bure, dishi,remote na vifaa vyote bure pamoja na kufungiwa king'amuzi hicho bure endapo mteja huyo atalipia kifurushi kikubwa cha Azam Play mwaka mzima.

Mteja wa Azam atatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 336,000 kwa mwaka ambapo ni sawa na kifurushi cha 28,000 cha Azam play kinachohusishwa na promosheni hii.

Mkuu wa Uwendeshaji wa Azam Media, Yahaya Mohamed amesema kuwa promosheni hii itamsaidia mteja kupata king'amuzi kipya na kuokoa kiasi cha shillingi 165,000 na kupata chaneli zaidi ya 100.

Mohamed amesema kuwa, kifurushi cha Azam Pure kina zaidi ya chaneli 45, Azam Plus Chaneli zaidi ya 65 na Azam Play  unapata chaneli zote zaidi ya 100 na kama mteja atatalipia hicho basi atapewa king'amuzi na kufungiwa bure.

Uamuzi huo unakuja ili kuleta maudhui ambayo yanakidhi haja na viwango kwa watanzania na kwakuwa Azam ipo Afrika Mashariki na Kati lakini wameamua kuanza na hapa nchini.

Mohamed amesema kuwa huduma hii itadumu kwa mwezi mmoja lakini itakuwa ni promosheni endelevu

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...