Tuesday, March 29, 2016

KESI UCHAGUZI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA KINONDONI IDD AZZAN YAPIGWA KALENDA.

 Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la kinondoni   haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda leo jijini Dar es Salaam.
Wakili mshitakiwa  Juma Nassoro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. juu ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni .Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akitoka Mahakani hapo mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CUF) iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Idd Azzan imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kuu ya Tanzania.

Juma Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa Kinondoni amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo amemuaomba msajili kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya kupangiwa tarehe nyingine.

Kwa upande wa Mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza  kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo  haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...