Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishukua kutoka kwenye gari lake la Ukuu wa Mkoa wakati alipokuwa akifika kwa mara ya kwanza ofisini kwake Dar es Salaam jana mchana.
Katibu Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.
Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli akisalimiana na Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akizungumza wakati wa kumakribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na RC Paul Makonda.
Wakuu wa Idara mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya kumpokea mkuu wao wa mkoa.
Mkutano ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, akimkabidhi kadi ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake.
……………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kazi rasmi jana mchana ambapo alifanya mazungumzo na wakuu wa idara na Vitengo mbalimbali na kutoa maagizo mazito ambapo alitoa masaa 24 kwa wakuu hao ya kumpa taarifa zilizopo katika maeneo yao husika zenye kuelezea changamoto mbalimbali ili kuona wananchi wanakabiliwa na changamoto zipi na namna atakavyoweza kuzitatua.
Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wakuu hao wa idara na vitengo katika hafla fupi ya kukaribishwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali ya wakuu hao wa idara na vitengo pia ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
Awali Makonda alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha yeye kushika nafasi hiyo baada ya Mheshiwa Rais Dk.John Magufuli kusikia sauti ya Mungu na kuifanyia kazi ya kumchagua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha Makonda alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika nyazifa hiyo muhimu ya kuwatumikia wananchi ambapo pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam wa zamani, Saidi Meck Sadiki kwa kumpokea akiwa kama Mkuu wa Wilaya na kumfundisha mambo mengi makubwa na mazuri ambayo yamemfanya kwa namna moja au nyingine kupata nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa.
Makonda amesema kwamba kwa sasa hajui chochote badala yake amewaomba watendaji wote kuonesha ushirikiano kati yao ili kuupeleka kwa kasi mkoa wa Dar es Salaam kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment