Tuesday, March 29, 2016

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI NA IDARA KUTUMIA KITUO CHA KUIFADHI TAARIFA CHA TAIFA


Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kuhifadhia taarifa zao.
Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi kwa usalama mkubwa wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumza na wadau hao juu ya matumizi ya kituo hicho kuhifadhia taarifa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza nawawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ili kuhifadhia taarifa zao.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya matumizi ya ‘National Information Data Centre’
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ili kuhifadhia taarifa zao. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura pamoja na Ofisa Mkuu Idara ya Ufundi TTCL, Senzige Kisonge wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Mkuu wa Idara ya Compyuta NSSF, Yahaya Madenge (kulia) akiuliza swali kupata ufafanuzi juu ya usalama wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi akiuliza kupata ufafanuzi juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kinavyofanya kazi na kumlinda mteja wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye tai ya mistari miekundu) akizunguka na baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali vitengo vya IT kuwaonesha miundombinu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ ilivyojengwa kisasa kumlinda mteja wake na taarifa zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Baadhi ya mashine kubwa za kisasa za kufua umeme katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitungi ya gesi ya kuzimia moto endapo ukitokea inayofanya kazi kwa kujiongoza yenyewe mara tukio la moto linapojitokeza katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi moja ya vyumba maalumu vya usalama katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi (kulia) moja ya mitambo ya kisasa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’.
Baadhi ya mashine zinazofanya kazi ya kupooza mitambo katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa ‘National Information Data Centre’ kuhifadhia taarifa zao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...