Shirika la la Nyumba linatarajiwa kushiriki katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani kitakachofanyika jijini Dar es Salaam kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samiah Suluhu Hassan, shughuli ambayo itaambatana na semina maalum kwa wanawake wote.
Wakizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, wandaaji wa tukio hilo, kutoka Kazi Services kwa kushirikiana na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) pamoja na wadau wengine, wa Shirika la Nyumba la Taifa, Benki ya NBC na Hoteli ya Serena.
Mkurugenzi wa Kazi Services, Bi. Zuhura Sinare Muro amebainisha kuwa, Wanawake zaidi ya 400, wanatarajia kushiriki kwenye tukio hilo ambalo pia kutakuwa na semina maalum ambayo itaendeshwa na wanawake mbalimbali ambao wameweza kuthubutu n ahata kufikia malengo katika nafasi ya mwanamke.
“Tukio la kesho ya siku ya mwanamke, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Ambapo pia wanawake hao zaidi ya 400 watashiriki katika tukio hilo litakaloenda sambamba na semina ambayo itatolewa na wanawake wenyewe ikiongozwa na Muongeaji Mkuu, Balozi Asha Rose Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN” amebainisha Bi. Zuhura Muro.
Bi. Zuhura Muro ameongeza kuwa, Maadhimisho ya mwaka huu yanabeba Utaifa kutokana na kada hiyo ya mwanamke kupata nafasi ya kipekee kwa Mwanamke kuwa kiongozi wa juu tokea zaidi ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania.
Aidha, amebainisha kuwa, baada ya kilele hicho, wanatarajia kuwa na mtandao mzuri wa wanawake kwa nchi nzima ili kuboresha vipaji vyao na waweze kuwa viongozi, watendaji na wanamama wazuri mahala pa kazi na ngazi za familia.
Tukio hilo linatarajia kufanyika kuanzia majira ya saa tisa alasiri, katika hoteli hiyo ya Serena jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment