Thursday, March 24, 2016

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JNIA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni wakati wa ziara yake katika Kituo hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...