Friday, May 16, 2008

Wahaini wa Pemba waachiwa



SIKU moja baada ya wazee wa Pemba walioshiriki kupeleka barua Umoja wa Mataifa kutishia kuwa watu 10,0000 waliiotia sahihi, watajisalimisha katika vituo vya polisi iwapo wenzao walikamatwa hawatoachiwa, wameachiwa kwa dhamana baada ya kuchukuliwa maelezo yao.

Akithibitisha hilo Kamishna wa Polisi Zanzibar Khamis Mohammed Simba alisema watu saba waliokuwa wamewashikilia katika vituo vya polisi kisiwani Unguja wamechiwa uhuru na kwamba watapewa usafiri wa kuwarejesha kwao Pemba.

“Ni kweli leo Ijumaa tumewaachia watu saba tuliokuwa tumewakamata na
tunaandaa utaratibu wa kuwarejesha kwao wote,” alisema. Kamishna.

Alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuwahoji na kukamilika kwa ushahidi wa awali na kuongeza kuwa iwapo kutahitajika maelezo zaidi watachukuliwa tena na kuhojiwa kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa bado uchuguzi unaendelea. Habari zaidi soma Mwananchi kesho.

Hata hivyo taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Marshed Ahmed Marshed (mtoto wa mmoja wa wazee waliokamatwa) zinasema kuwa wapemba hao hawajaachiwa mpaka sasa bali ni janja ya serikali iliyofanya na Usalama wa Taifa kujaribu kuficha ukweli.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...