Sunday, May 25, 2008

Bemba anaswa Ubelgiji



THE HAGUE, Uholanzi
MMOJA wa makamu wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean Pierre Bemba amekamatwa hii jana nchini Ubelgiji.

Kiongozi huyo wa chama cha Movement for Liberataion of Congo MLC anashikiliwa kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita vilevile uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kwa mujibu wa Beatrice le Fraper mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Bwana Bemba alikamatwa juzi jioni mjini Brussels.

Mahakama hiyo inataraji kuwa Bemba atafikishwa mahakamani nchini humo Ubelgiji katika kipindi cha siku chache zijazo kisha kuhamishwa kwenye mahakama ya ICC majuma machache yatakayofuatia.

Hati ya kukamatwa kwa Jean Pierre Bemba ilitolewa tarehe 16 mwezi huu wa Mei japo kiongozi huyo wa zamani hakuwa na taarifa yoyote kwani hatua hiyo haikutangazwa hadharani.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...