Sunday, May 18, 2008

Kumekucha vijana CCM



KINYANG'ANYIRO cha kugombea Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), kimeanza kushika kasi, baada ya mmoja wa wanachama wake maarufu, Hussein Mohammed Bashe, kujitokeza na kutangaza rasmi nia yake ya kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 13, mwaka huu.

Bashe (30), ambaye ana Shahada ya Kwanza ya Biashara na Masoko kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, mkoani Morogoro, alitangaza nia yake hiyo alipozungumza na waandishi wa habari, katika ukumbi wa Millenium Towers, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema amefikia hatua hiyo, ili apate fursa ya kupambana na changamoto zinazoikabili UV-CCM kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini na duniani na kusababisha ishindwe kukidhi mahitaji na matarajio ya vijana wa Kitanzania kwa nyakati za sasa, habari ya Muhibu Said

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...