Thursday, November 15, 2007

Nyama ya nyoka ni tamu!!!

Na Nora Damian wa Mwananchi

UBISHI makali ulizuka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana wakati wa mahojiano kati ya Wakili Gabriel Mnyele kwa upande wa wadaiwa na shahidi wa pili Daudi Kamugisha (40) kwa upande wa wadai katika kesi ya madai ya kashfa ya inayosikilizwa na Jaji Augustino Shangwa.

Katika kesi hiyo, wadai ni waumini wa dhehebu la Katoliki wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Afrika, wanaopinga habari iliyoandikwa Mei 29 mwaka 2005 katika gazeti la Majira zikidai kuwa wafuasi wa shirika hilo wanalazimisha kuwinda na kula nyama ya nyoka na kutembea pekupeku.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, anayayedaiwa kuwashurutisha wafuasi hao ni mwanzilishi wa shirika hilo, Padre Riccarido Enrico, mwenye asili ya Italia ambaye sasa ni raia wa Tanzania na amekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka 20 akitoa bure huduma za elimu ya sekondari mbali na huduma za kiroho. Soma MWANANCHI kwa taarifa zaidi

No comments:

TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini CHUNYA Ikiwa ni mkakati wa  k...