Friday, November 23, 2007
Tiba MOI:Aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa, afariki
Jackson Odoyo na Andrew Msechu wa Mwananchi
EMMANUEL Mgaya (19), aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa Jumatatu wiki hii baada awali kufanyiwa wa mguu kimakosa, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), amefariki dunia jana asubuhi.
Mara baada ya Mgaya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kisha kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hadi mauti yalipomfika jana saa 2:30 asubuhi.
Awali Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na Emmanuel Didas ya kichwa badala ya mguu, Novemba mosi mwaka huu katika taasisi hiyo.
Akizunguza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu muda mfupi baada ya Mgaya kufariki dunia, mmoja wa wauguzi wa MOI, alisema hali ya mgonjwa huyo, ilianza kuwa mbaya juzi mchana. Soma MWANANCHI kwa taarifa zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment