Tuesday, November 13, 2007

Breaking Newsss

RAIS Jakaya Kikwete ameteua wajumbe wa Kamati ya uangaliaji upya mikataba ya uchimbaji wa madini nchini itakayo kuwa na jukumu la kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi ya mikubwa nchini.

Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe kumi na mmoja itakuwa chini ya Uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine ni pamoja na:-

Zitto Kabwe- Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA),
John Cheyo -Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP),
Salome Makange- Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini
Mugisha Kamugisha- Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha
Edward Kihundwa- Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi
Dk. Harrison Mwakyembe- Mbunge wa Kyela (CCM)
Ezekiel Maige- Mbunge wa Msalala (CCM)
Peter Machunde- Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE)
David Tarimo- Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Shirika la Kimataifa la CoopersHouse
Maria Kejo- Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria

Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi ilisema kuwa pamoja na mambo mengine kamati hiyo pia itakuwa na kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.

Kamati hiyo iliyopewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi yake pia inajukumu la kukutana na chamber of minerals na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo.

Kuundwa kwa Kamati hiyo kunafuatia hoja binafsi ya mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa kamati itakayochunguza mikataba ya madini kufutia Waziri wa Nishati, Nazir Karamagi kutia saini makubalino ya uchimbaji wa madini katika mgodi wa Buzwagi akiwa nje ya nchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...