Thursday, November 15, 2007

Eti Bunge kuamshwa kwa wimbo wa Taifa

Na Muhibu Said wa Mwananchi aliyepo Dodoma

BUNGE la Jamhuri ya Muungano, limeridhia mabadiliko ya kanuni zake ambapo sasa vikao vya kwanza na vya mwisho vya mkutano wake, vitakuwa vikianza kwa wimbo wa taifa kabla ya kusoma dua na pia vitakuwa vikifungwa kwa kufuata utaratibu huo.

Katika mabadiliko hayo, Spika na Naibu wake watakuwa wakiapa viapo vilivyowekwa kwa mujibu sheria, viongozi wa Bunge wanaokalia kiti cha Spika kuendesha shughuli za Bunge kwa haki bila upendeleo, Bunge kutambua haki ya raia ya kujitetea na kujisafisha kutokana na kauli zinazotolewa bungeni na Kamati za Bunge kufanya kazi zake kwa uwazi.

Pia Kamati za Hesabu za Serikali na za Serikali za Mitaa, zitakuwa na wenyeviti kutoka Kambi ya upinzani bungeni, Bunge litakuwa na Mshauri Mkuu wa Mambo ya Sheria, wenyeviti wa Bunge watakuwa watatu badala ya wawili wa sasa na uchaguzi
wao utazingatia jinsia na pande za Muungano.

Mabadiliko hayo pia yanahusu kanuni ya kutosema uongo bungeni kufanyiwa marekebisho, taarifa za kamati za kudumu za Bunge kuwasilishwa na kujadiliwa bungeni, pia kuweka mpangilio mzuri, kuunganisha baadhi ya kamati hizo pamoja na majukumu yake
na kuziweka chini ya Nyongeza ya Sita, kuweka utaratibu mzuri kuhusu usalama wa maeneo ya Bunge na Bunge kuwa na uwezo wa kuamua iwapo Muswada wowote wa Sheria unaowasilishwa kwa dharura unastahili kupitishwa na Bunge kidharura. Kwa taarifa zaidi soma MWANANCHI

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...