Tuesday, November 20, 2007

Mambo ya Kusini sasa safi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  alikagua barabara  ya Lindi – Kibiti hadi Mingoyo pamoja na Daraja la Mbwemkuru, wakati akitoka Lindi kwenda  Kilwa.

Kabla ya ukaguzi huo, Rais alipata taarifa ya maendeleo ya barabara hii muhimu kwa mikoa ya kusini na Daraja la Umoja (ambalo hakulikagua) kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Bw. Omar A. Chambo; ambaye amemueleza Rais kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa barabara hiyo.  Ujenzi wa barabara ambao unafanyika kwa awamu, utakamilika mwishoni mwa mwaka huu wakati Daraja la Umoja linatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwaka 2008. 

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,

20 Nov, 07.

 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...