Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura Jimbo la Kilombero wametakiwa kuhakikisha wanatoa Kipaumbele kwa wapiga kura wenye Mahitaji Maalumu pindi watakapofika Kituoni siku ya Uchaguzi Mkuu Tarehe 29 Oktoba 2025.
Rai hiyo Imetolewa Leo tarehe 26 Oktoba 2025 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilombero Bi. Joha Mlindwa wakati akifungua Mafunzo ya Siku Mbili kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura yanayofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba uliopo Ifakara.
" Ninyi ndio watendaji mnaokutana na wapiga kura, hivyo hakikisheni mnazingatia unadhifu, lugha nzuri na kutoa Kipaumbele kwa wapiga kura wenye Mahitaji Maalumu pindi watakapofika Kituoni kama Wajawazito, Watu wenye ulemavu, Wazee n.k ". Alisema Bi. Joha Mlindwa
Aidha Bi. Joha Mlindwa aliwasisitiza Wasimamizi katika Vituo kuhakikisha Wanazingatia kwa Umakini Katiba, Sheria, Kanuni ,Miongozo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi .
"Tangu siku ya Uteuzi wenu Ninyi ni Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mtawajibika kwa Tume na sio kwa mamlaka nyingine katika Utekelezaji wa Majukumu yenu ya Uchaguzi hivyo mzingatie Mafunzo mtakayopewa". Alieleza Bi. Joha
Aidha Wasimamizi hao walikula Kiapo cha Kutunza Siri na Tamko la Kujitoa uanachama wa Chama cha Siasa au kutoka Mwanachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kilombero Bi. Joha Mlindwa.
Mmoja wa Wasimamizi hao wa Vituo vya Kupigia Kura wanaopatiwa Mafunzo Bi. Yasinta Victor alisema kuwa wanazingatia Viapo walivyokula na maelekezo yote watakayopewa na Tume ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu Tarehe 29 Oktoba 2025.
Mafunzo hayo yanajumuisha Wasimamizi wa Vituo 597 na Wasimamizi Wasaidizi 1194 katika Vituo 597 Vilivyopo Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara.





.jpeg)





No comments:
Post a Comment