Sunday, October 05, 2025

SEGEREA YAITIKA! VIJANA WAJITOKEZA KWA WINGI KUMPONGEZA DK. SAMIA NA BONNAH KAMOLI 🏃‍♀️🇹🇿










Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Maelfu ya vijana, wadau wa michezo na viongozi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kushiriki mbio za jogging na Tamasha la IJA Festival Season 1 lililofanyika katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo limebeba ujumbe maalum wa kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwa amani na kumchagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli.

Akizungumza katika tamasha hilo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, aliwataka vijana na wanamichezo kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba mwaka huu kupiga kura kwa amani na kumchagua Dk. Samia, akisisitiza kuwa Rais huyo amekuwa mdau mkubwa wa michezo na maendeleo ya vijana.

“Ilani ya CCM inatambua umuhimu wa michezo kama ajira. Dk. Samia amethibitisha kwa vitendo upendo wake kwa michezo na maendeleo ya vijana. Oktoba 29, kila mmoja ajitokeze kupiga kura – kura yako ni sauti yako kwa maendeleo,” alisema Chatanda.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwatuliza vijana dhidi ya uvumi wa maandamano, akisisitiza kuwa hakuna wa kuwazuia wananchi kutumia haki yao ya kikatiba.

“Msiogope, uchaguzi ni haki yenu. Hakuna atakayefanikiwa kuwatisha Watanzania walioamua kuendeleza amani,” alisisitiza Chatanda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohammed, aliwahimiza vijana wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpa kura za heshima Rais Dk. Samia, akisema:

“Vijana wa Dar es Salaam tumejionea kazi kubwa ya Rais wetu. Sasa ni wakati wa kumrudishia heshima kwa kura zetu.”

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, aliwashukuru Umoja wa Vilabu vya Jogging Wilaya ya Ilala kwa kuandaa tamasha hilo lililopambwa na burudani kutoka kwa nyota wa muziki nchini, akisema linaonesha umoja, amani na mshikamano wa vijana.

“Oktoba 29 tujitokeze kwa wingi kumchagua Rais Dk. Samia, mimi kama Mbunge wa Segerea, na madiwani wote wa CCM. Pamoja tunaijenga Segerea yenye maendeleo,” alisema Bonnah.

Tamasha hilo limeonesha namna michezo inavyoweza kutumika kama jukwaa la kukuza afya, umoja na hamasa ya maendeleo ya taifa, likiwa sehemu ya mwamko mpya wa vijana kuelekea uchaguzi wa mwaka huu.

🌟 Segerea inasema: Kura ni maendeleo, amani ni nguvu yetu! 🇹🇿

#SegereaYaitika #DkSamiaSuluhu #BonnahKamoli #IJAFestival #CCMTanzania #VijanaWaMichezo #Uchaguzi2025 #TanzaniaInajengwa

No comments:

TANZANIA YAIPONGEZA NORWAY KWA KUENDELEA KUUNGA MKONO MAENDELEO

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameipongeza Serikali ya Ufalme wa Norway kwa ...