Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Petro Magoti, ameongoza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya katika mazoezi ya pamoja yaliyolenga kuimarisha afya na ustawi wa mwili. Mazoezi hayo yamefanyika kwa lengo la kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile presha, kisukari, unene uliopitiliza (obesity) na mengineyo yanayotokana na kukosa mazoezi ya mara kwa mara.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Mhe. Magoti amesisitiza umuhimu wa viongozi na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki ili kudumisha afya njema, kuongeza ufanisi kazini, na kupunguza gharama za matibabu.
Amesema kuwa afya bora huanza na maamuzi madogo ya kila siku, na kwamba kufanya mazoezi ni njia rahisi, ya bure na yenye manufaa makubwa kwa maisha ya kila mtu.
Mazoezi hayo yamepambwa na hamasa kubwa kutoka kwa washiriki, yakidhihirisha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kujenga jamii yenye afya bora na yenye tija.
#MazoeziNiAfya #Kisarawe #DCMagoti #AfyaBoraKwaWote #PamojaTunaweza
No comments:
Post a Comment