Wednesday, August 13, 2025

*WAZIRI MKUU AKAGUA MABASI, MIUNDOMBINU YA MRADI WA BRT AWAMU YA PILI







WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 13, 2025 amekagua mabasi mapya kwa ajili ya awamu ya pili mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT-2) pamoja na miundombinu ikiwemo kituo kikuu cha mabasi hayo cha Mbagala Rangi tatu na kituo cha gerezani, jijini Dar es Salaam.

Katika ukaguzi huo, Mheshimiwa Majaliwa ametembelea ujenzi wa kituo maalum cha kujazia gesi kwa ajili ya mabasi hayo, kinachojengwa katika kituo cha Mbagala Rangi Tatu.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Waziri Mkuu amewaagiza waendeshaji wa mradi huo kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha maeneo yaliyobaki yatakayowezesha mradi huo kuanza kutoa huduma ndani ya mwezi huu.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu aliambana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Zainab Katimba, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi pamoja na watendaji wengine wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT).

Mradi wa BRT-2 unatarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri wa umma jijini Dar es Salaam na kutoa huduma ya kisasa, salama na ya haraka kwa wananchi.


No comments:

*WAZIRI MKUU AKAGUA MABASI, MIUNDOMBINU YA MRADI WA BRT AWAMU YA PILI

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Agosti 13, 2025 amekagua mabasi mapya kwa ajili ya awamu ya pili mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT-2) pa...